WITO WA MKUTANO MKUU WA KWANZA WA SHIRIKISHO LA WAAFRIKA (UMAJUMUI)

Je, unaamini kwamba umoja wa kisiasa wa mataifa ya Kiafrika ni jambo la dharura kwa Waafrika wote waishio katika Bara letu na nje (Diaspora)?

 Je, unakubaliana na Kwame Nkrumah aliposema kwamba: "Ni dhahiri kwamba ni lazima tupate ufumbuzi wa Kiafrika kwa matatizo ya  Afrika;  hii inaweza kupatikana tu katika umoja wa Afrika. Tukigawanyika tunakuwa wadhaifu; Tukiunganika Afrika inaweza kuwa moja miongoni mwa mataifa makubwa duniani, kwa maendeleo ya binadamu "?

 Je, unakubaliana na Cheikh Anta Diop aliposema: “Umoja wa  Afrika utatokana na wananchi wenyewe, kupitia vuguvugu la kupambana na unyonge wa kisiasa na kiuchumi ulioenea katika bara letu. Kwani unyonge wetu unatokana na udhaifu wa watawala katika kutatua matatizo yanayotukabili, hivyo hapana budu wananchi wasimame kidete ili kuleta maendeleo yao. Wananchi watapaswa waelewe kuwa unyonge wao unaendana na udhaifu wa watawala. Nina hakika kuwa umma wa  Afrika utazaa viongozi wapya miongoni mwa vijana wao, wenye ari na moyo wa kuanzisha vuguvugu la maendeleo katika bara letu. Vuguvugu hili litabomoa ukuta unaozuia muungano wa bara zima la  Afrika”?

 Je, wewe umechoshwa kuona Waafrika wakiwa wanyonge wasioweza kukabiliana na majanga yaliyosababishwa na watu?

 Je, wewe unaamini kuwa Uafrika wetu unapaswa kuwa nguvu yetu na wala siyo mzigo?

 Je, wewe unaamini kuwa katika  Afrika tuna haja ya kuwa na uongozi imara wenye nguvu itakayothubutu kudai fidia kwa ajili ya ukandamizaji na unyonyaji tuliofanyiwa chini ya ukoloni na utumwa?

 

Kama umejibu ‘ndiyo’ angalao kwa suali moja kati ya haya yaliyoulizwa, basi tafadhali eneza wito huu kwa wenzio ili watembelee tovuti hii na kujitayarisha kuhudhuria mkutano mkuu wa kwanza wa UMAJUMUI wa  Afrika (African Federalists Congress) http://www.africanpublius.com 

 Tunategemea kushirikiana nawe pamoja na mamilioni ya Waafrika katika kuunda shirikisho la UMAJUMUI wa  Afrika (Pan African Federalist Movement) ambao utaunganisha bara letu la  Afrika katika muda mfupi wa kizazi kimoja. Unawea kuwasiliana nasi kwa kutumia anuani hii: africanfederalist@gmail.com

 Tafadhali toa mchango wako wa mawazo katika kuandaa mkutano huu mkuu wa kihistoria

Sote tushiriki ili kufanikisha Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Shirikisho la Umajumui wa  Afrika

 Lengo letu ni kuanzisha harakati ili hatimae tuweze kuunda Umoja wa Mataifa ya Kiafrika.

 Unawezaa pia kuwasiliana na wafuatao:

Mamadou Ndoye - simu ya mkononi: +221-77 130 17 24 - barua pepe: mam.ndoye@gmail.com

Mamadou Diouf Mignane - simu ya mkononi: +221-77 632 68 80 - barua pepe: midiouf@yahoo.fr